New Lyrics

LINEX SUNDAY MJEDA – Kesho Yangu Lyrics

LINEX SUNDAY MJEDA - Kesho Yangu Lyrics
LINEX SUNDAY MJEDA – Kesho Yangu Lyrics

LINEX SUNDAY MJEDA – Kesho Yangu Lyrics Niliangamia kwa kukosa maarifa
Hofu ya Mungu tena nikaiweka kando
Sikuogopa hata kufa aah
Nyota ya umaarufu ikafifia

Ikafanya —-
Maombi yangu hayajibiwi
Hata nifunge na kusali ii

Nikajiona natembea peke yangu
Amenigeuzia shingo oo
Mpaka muumba wangu

Nilikata tamaa
Nikajiona nipo kwenye msitu na sisikii
Hata hesabu za watu
Jitokeze tukuone
Tukupe manung’uniko yetu

Siogopi leo naihofia kesho yangu
Mungu wangu uliye juu
Badilisha maisha yangu
Nami nitembee nikiringa nikitamba
Nikiwa na uhakika wa maisha yangu

Mungu umekuwa msiri wangu
Miaka nenda rudi
Hata nikiwa uchi
Huchoki kunisitiri

Kwani mi ni nani?
Unipe dhamani ya juu
Uniepushe na maadui zangu

Na kwani mi ni nani?
Unionyeshe upendo wa hali ya juu
Unilinde usiku na mchana

Leo hawazungumzii
Matunda ya wema unaowatendea
Wanazungumzia jaribu
Ya maisha yao yanapoyumba

Siogopi leo naihofia kesho yangu
Mungu wangu uliye juu
Badilisha maisha yangu
Nami nitembee nikiringa nikitamba
Nikiwa na uhakika wa maisha yangu

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button